-->

Joanita: Filamu Zetu Unaangalia Hata na Mkweo

Fatuma Makame ‘Joanita’

Fatuma Makame ‘Joanita’

Msanii wa ‘long time’ kwenye ulimwengu wa uigizaji Bongo, Fatuma Makame ‘Joanita’ amesema kuwa, filamu zinazoandaliwa na kampuni inayoandaa na kusambaza filamu ya Hamdombe zinaangalia maadili kiasi kwamba, unaweza kuangalia ukiwa na mwanao au mkweo.

Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Joanita alisema kuwa wameona ni vyema kuandaa filamu za aina hiyo ili kutoharibu jamii lakini pia kuelimisha na kuburudisha bila kujali rika kama itakavyokuwa kwenye filamu yao mpya itakayotoka baada ya Krismas ya Nitakufa Kwa Ajili Yako.

“Hamadombe tunajali maadili, filamu zetu ambazo tunaandaa na kusambaza wenyewe zinakidhi maadili ya Kitanzania, huwezi kukutana na scene chafu na ndiyo maana jamii imetukubali haraka,” alisema Joanita.

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364