-->

Jide Ahamia Ujerumani!

LADYJAYDEE

MOYONI nina majonzi, sina tofauti na mpofu! Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ au ‘Lady Jaydee’ kwa sasa hana makazi maalum Bongo, amehamishia makazi na shughuli zake katika ardhi ya ‘Kansela’ wa Ujerumani, Angelina Merkel kwenye Jiji la Born.

Katika mazungumzo yake na mwandishi wetu kwa njia ya simu, Jumatatu ya wiki hii, Jide ambaye alidai kwa sasa yupo nchini kwa Sikukuu ya Krismasi (kesho), alisema sababu zilizomfanya akapige kambi nchini humo ni kuchoshwa na maneno ya watu ambao kazi zao ni kutazama nani kafikwa na baya ili waeneze sumu ya maneno.

Kwa sauti ya ‘kibabe’ na yenye mamlaka, Jide alisema: “Lakini ukiachana na Ujerumani, wakati mwingine natumia muda mwingi kuwa nchini Afrika Kusini (Sauzi) kwa mizunguko ya kimaisha na kupumzisha akili yangu.”

UJERUMANI ANA NYUMBA?

Jide: “Kwa sasa naishi hotelini, lakini kuna marafiki na jamaa zangu ambao wako kule. Kwa hiyo sina shida. Muhimu ni kukaa mbali na maneno ya watu wafurahiao matatizo ya wengine.

Kila mtu anageuka adui, ukiwa na mafanikio makubwa, watu wanajisogeza karibu, ukipungukiwa na jambo, haohao wanaanza maneno na kukusema vibaya, maisha hayatabiriki.”

HATAKI KUSIKIA MAPENZI!

Amani: “Vipi kuhusu mumeo, Gardner Habash, una mpango wa kurejeana naye?”

Jide: “Sitaki kusikia kabisa mambo ya mapenzi. Sitaki na usiendelee kuuliza upuuzi kama huo tafadhali. Si tu kwa huyo mtu (Gardner), hata kwa awaye yeyote, sitaki kusikia.”

ASIULIZWE KUHUSU MALI ZAKE!

Amani lilimuuliza Jide kuhusu ukweli juu ya madai kwamba amefilisika na kufikia hatua ya baadhi ya nyumba zake kuwa katika hatihati ya kupigwa mnada.

Jide: “Sitaki kugusia mambo hayo. Hata hivyo, umebahatika sana kupokelewa simu na kuzungumza na mimi, licha ya kuwa umejitambulisha unatoka Global. Sipendi mazungumzo na waandishi, hususan nyie wadaku.”

KUHUSU MUZIKI?

Jide: “Siwezi kusema nimeacha muziki, nipo maana ndiyo kazi pekee iliyonitambulisha.

Nawaasa mashabiki wangu waendelee kiniunga mkono, nawapenda sana na bila wao hakuna Jide. Lakini kwa sasa kuna mambo nayaweka sawa nje ya muziki.”

YUPO DAR AU KWINGINEKO?

Jide: “Kwa sasa niko Dar (Jumatatu), lakini keshokutwa (jana

Jumatano) nitakuwa nyumbani Musoma kwa ajili ya Krismasi. Niko kwenye mapumziko maalum ya sikukuu hiyo, lakini baada ya hapo, nitaendelea na mambo yangu mengine, ikiwemo kurejea Ujerumani.”

Chanzo: GPL

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364