-->

Johari Awewesekea Penzi la Mbunge

MUIGIZAJI mkongwe wa filamu Bongo, Blandina Chagula anayefahamika kisanii kama Johari, anadaiwa kuwewesekea penzi la mbunge mmoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (jina linahifadhiwa) ambaye alifunga ndoa miezi michache iliyopita.

JOHARI342

Chanzo makini kilicho karibu na msanii huyo kimeliambia gazeti hili kuwa Johari alikasirishwa na kushangazwa na hatua ya msanii mwenzake kuolewa na mbunge huyo, ilihali akijua kuwa yeye aliwahi kuishi naye kimapenzi, ingawa alikataa kuolewa naye kwa kile alichosema ‘hajatulia’.

“Johari anaweweseka kweli jamani, yaani kinachomuuma huyo mke wa mheshimiwa ni yeye ndiye aliyemkutanisha na anajua kila kitu, lakini anashangaa hata ilivyokuwa hadi akakubali kuolewa naye, yaani ni kama mtu aliyeumia sana,” kilisema chanzo hicho ambacho kiliomba hifadhi ya jina lake ili kulinda ushoga wao.

Baada ya kunasa ushahidi unaothibitisha Johari akimzungumzia mbunge huyo kuonesha anaweweseka, gazeti hili lilimtafuta Johari na kumwuliza kuhusu tuhuma hizo, lakini msanii huyo aliruka kimanga, akidai hajawahi kuweweseka kwa penzi la mbunge huyo na wala hajawahi kuwazungumzia.

Chanzo: GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364