-->

Nitamdunda Shetta Zaidi ya Mr Nice – Dudubaya

Msanii wa muziki Dudubaya amefunguka na kusema kuwa msanii Shetta asitake kumchokoza na kumrudisha katika enzi za nyuma cha msingi anataka aache mara moja kutumia jina lake la Mambaambalo yeye ndie alianza kulitumia toka mwaka 2007.

Dudubaya na Sheta

Dudubaya alisema hayo kupitia kipindi cha Planet bongo na kusema kuwa Shetta kwake ni kama mjukuu tu kwani yeye alianza kutoka wakati muziki wanarekodi kwa shilingi elfu kumi kwa hiyo baada ya hapo walikuwa wanamuziki kama kina Stara Thomas, Lady Jaydee,baadae wakaja wakina Marlaw,Bushoke, Matonya na wengine baadae sana ndio wanakuja wao hivyo kwake ni kama mjukuu.

“Imeniudhi sanaa Shetta kutumia jina langu la ‘Mamba’ hawezi kujiita Mamba wakati mimi jina langu toka 2007, hawa watoto sometimes wanakosa adabu, sitaki atumie jina langu na akiendelea kutumia hilo jina asinirudishe kwenye enzi za Mr Nice, Nitamfanya zaidi ya Mr Nice” Alisema Dudubaya

Lakini Dudubaya aliendelea kusema kuwa amechukua jitihada za kumpigia simu Shetta lakini hajafanikiwa kumpata kwenye simu lakini alikuwa anataka kumueleza kuwa akome kutumia jina lake, na kusema kuwa kwanza yeye Shetta hafai kujiita Mamba labda ajiite Kenge.

“Mamba ni jina langu mimi na ndio maana biashara zangu hata nikifungua Pub inaitwa Mambaz, nikifungua chochote kinaitwa mamba hivyo hawezi yeye kujiita mamba, kwanza umbo lake lenyewe siyo mamba yule ni Kenge, suala la mimi kukaa kimya kwenye muziki nina shughuli zingine za kufanya ila ni jina langu mimi, huwezi leo DMX au Jarule amekaa kimyaa kwenye muziki wewe unaibuka unajiita Jarule utakuwa bumbuwazi” Alisema Dudubaya

Eatv.tv

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364