-->

Johari, Baba Haji Wagandana

IMG_5612

Mastaa wawili wa Bongo Muvi, Super Woman, Blandina Chagula ‘Johari’ na mwenzake, Adam Haji ‘Baba Haji’ wakiwa katika pozi baada ya kukutana usiku mnene kwenye Hoteli ya Rodizio iliyopo Masaki jijini Dar.

Musa Mateja, Risasi jumamosi
Dar es Salaam: Mh! Mastaa wawili wa Bongo Muvi, Super Woman, Blandina Chagula ‘Johari’ na mwenzake, Adam Haji ‘Baba Haji’ wamebambwa wakiwa wamegandana kwa dakika kadhaa kwa madai ya ‘kumisiana’ kwa muda mrefu.
Ishu hiyo iliyopigwa chabo na paparazi wetu ilijiri usiku mnene kwenye Hoteli ya Rodizio iliyopo Masaki jijini Dar kulikokuwa na shughuli iliyoandaliwa na mastaa wa Bongo Muvi ya kumpongeza Paul Makonda kwa kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar na Rais Dk. John Pombe Magufuli.

IMG_5615

Wakiendelea kufanya yao.

Baada ya kukutana, wawili hao walikumbatiana kwa dakika kadhaa kisha kila mmoja ‘alijibebisha’ kwa mwenzake huku wakinong’ona na kutoa vicheko vilivyowafanya mastaa wenzao kuwageukia na kuibua gumzo.
“Jamani kulikoni Johari leo kaja kwenye shughuli? Siyo kawaida yake na hivi anavyogandana na Baba Haji kila mtu anamkodolea macho,” alisikika mmoja wa wasanii chipukizi wa filamu.

IMG_5604

Wakishtuka baada ya kuona mwanga wa kamera.

Hata hivyo, Johari alipoona mwaga wa kamera ya gazeti hili unammulika yeye na Baba Haji alishtuka na kupiga mkwara kuwa hicho ndicho huwa kinamfanya anashindwa kwenda kwenye shughuli za mastaa.

“Sasa…(anamtaja paparazi wetu), picha zote hizo za nini? Kwanza ninyi ndiyo mnanifanya nisiwe nahudhuria kwenye matukio ya mastaa,” alisema Johari huku Baba Haji akiishia kucheka kisha wakatengana wakati wa kupiga picha na Makonda.
Shughuli hiyo iliyohudhuriwa na mastaa kibao ilimalizika mishale mibaya huku Johari na Baba Haji kila mmoja akitimua kivyake.

GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364