-->

Nilinusurika Kifo Mara Mbili-Kajala Masanja

STAA wa filamu za Bongo, Kajala Masanja, amesema aliwahi kunusurika kifo kutokana na kupata mshtuko mara mbili mara, baada ya kutoka selo alikokuwa akituhumiwa katika kesi ya kuuza nyumba kwa wizi.

Kajala alisema labda leo asingekuwa hai kama angeendelea kufuatilia matusi na lawama za mashabiki wake alizozikuta mitandaoni baada ya kutoka kwenye kesi hiyo.

“Sikuwa nikijua kinachoendelea huko mitandaoni, nilipotoka selo nikakutana na matusi ya kila namna, sikuweza kuyavumilia, wakati wote nilikuwa nikilia na kujutia kutoka selo, nilitamani hata nirudi huko lakini haikuwezekana.

“Kutokana na kuumia huko nikajikuta mara mbili tofauti nikizidiwa kwa kupata mshtuko wa moyo ambapo nilikimbizwa hospitali nikiwa sijitambui, nilitundikiwa chupa ya maji, lakini hali hiyo iliendelea hadi nilipokuja kuonyeshwa watu waliokuwa wakinitumia meseji hizo za matusi ndipo mapigo ya moyo yakarudi kawaida,” alieleza Kajala.

Kajala aliongeza kwamba alipogundua kwamba waliokuwa wakimtumia matusi kwenye mitandao ya jamii ni kikundi cha wasichana wanaofanya biashara ya miili yao na hajui kwanini walifanya hivyo, hapo ndipo alipoanza kuwa na moyo wa ujasiri akaanza kupuuza mambo ya mitandaoni.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364