-->

Msimpangie Beckham- Fid Q

Farid Kubanda ‘Fid Q’ ameshindwa kuwavumilia wabongo wanaomtusi mwanasoka David Beckham aliyeko nchini Tanzania mapumzikoni, kwa kuwaambia wasimpangie kutangaza bali wamuheshimu mtalii huyo ambaye ametumia garama zake kufika nchini na siyo ufadhili.

Fid Q amelazimika kufunguka hayo kwenye Stori tatu ya planet Bongo ndani ya East Africa radio baada ya watanzania kuanza kumshambulia mitandaoni mchezaji huyo kwanini hajitangazi kama yupo nchini kwenye mitandao wakati anapoweka picha kwenye mitandao ya kijamii.

Msanii huyo amesema kwamba watu wanatakiwa kuheshimu mipango ya mtu anapokuwa amesafiri kwa ajili ya kwenda mapumzikoni kwani hutumia muda mwingi katika maandalizi tofauti na watanzania kwa jinsi wanavyokurupuka.

“Wenzetu wakiwa wanajiandaa kwenda ‘Vaccation’huwa hawakurupuki kama sisi kwamba ukipata hela ndo unaondoka, wao wanakaa chini wana-plan kwamba labda mwakani nitaenda Tanzania nitaenda hapa na pale hivyo ni vyema wakajaribu kutulia kumuacha mtu afurahie utalii na arudi kwao salama” – alisema Fid

Pamoja na hayo Fid ameongeza “Kumtangaza Beckham kwamba yupo nchini kwetu ni makosa kwa sababu mtu huyu ni mkubwa na maarufu sana ana mashabiki lakini pia ana maadui vile vile. Kujitangaza kwamba ni promo na wakati sisi hatujamgharamia kuja na wala hajaletwa kwa ufadhili. tumuache afurahie mapumziko yake, na hata kupunguza ukali wa maisha” Fid aliongeza.

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364