-->

Kala Jeremiah: Baba Alifariki Siku ya Kukutana

MSANII wa miondoko ya hip hop, Kala Jeremiah, amesema hatasahau siku alipopanga kukutana na baba yake mzazi kwa mara ya kwanza kwani ndiyo siku aliyofariki dunia.

kala322

Kala Jeremiah

Kala alisema alitoka Mwanza hadi Dar es Salaam kumtafuta baba yake lakini kabla hajakutana naye alipokea taarifa mbaya kuhusiana na baba yake huyo jambo ambalo anadai halitatoka katika kumbukumbu za maisha yake.

Kala aliliambia MTANZANIA kwamba, tangu kuzaliwa kwake hajawahi kumuona baba yake huyo ndipo alipoamua kusafiri hadi Dar es Salaam kwa ajili ya kumtafuta na kuonana naye kwa mara ya kwanza.

“Niliumia sana kwanza ndiyo nilikuwa nakuja kumuona kwa mara ya kwanza ukizingatia tangu kuzaliwa kwangu sijawahi kumuona,” alieleza Kala.

Kala aliongeza kwamba, huenda kilichomchelewesha kuonana na baba yake ni ugumu wa usafiri kipindi hicho maana alilazimika kulala njiani kutokana na ratiba za mabasi kipindi hicho.

“Ilinilazimu kulala njiani ndipo siku ya pili nikafika Dar es Salaam, lakini nilipoanza kwenda kwa ajili ya kuonana na baba yangu nikapokea taarifa kwamba amefariki, iliniuma sana na sitaisahau siku hiyo na tukio zima lakini ndiyo mipango ya Mungu,” alisema Kala kwa masikitiko.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364