-->

TID Ampa Makavu Dully Sykes

Akiongea kwenye Planet Bongo ya East AFrica Radio, TID amesema Dully Sykes hakupenda kitendo cha Joh Makini kuwepo kwenye collabo yao ya wimbo wa confidence.

dully3

“Kwanza ile ngoma mwenyewe ndio alitaka kuwepo baada ya kuisikia, akasema mnyama hii ngoma kali naomba niweke sauti na mimi, nikamkubalia tukarekodi, lakini alivyokuja kusikia Joh Makini yupo akanipigia simu tena usiku, akaanza kunifokea, tena imagine ngoma yangu ananifokea..TID vp unaweka watoto wa Arusha? ndo unafanya nini?” , alisema TID,

TID aliendelea kwa kusema kuwa licha ya hilo baada ya kuandaa show ya ku-launch audio, alivyoona na Joh Makini anaperfom, akampigia Joh akimwambia asikubali kufanya show bila kumlipa.

“Baada ya hapo akampigia Joh akamwambia Joh ile show kubwa usikubali kuperfom bila kukupa milioni tatu, baadaye Joh akaniambia kwamba bila mkwanja haparfom, nikamuuliza we habari hizo umezitoa wapi? akaniambia ni Dully kanambia, nikamwambia ungejua huyo Dully alimind kusikia we upo kwenye ngoma! bahati nzuri siku Dully ananipigia kina nNicotrak walisikia”, alisema TID.

TID aliendelea kusema kuwa Dully ana mambo ya kitoto hivyo anahitaji kuacha ushindani usiokuwa na faida, na kushindana kikazi.

eatv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364