Kamati ya Bunge Kujadili Usalama wa Nchi -VIDEO
Dodoma. Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama leo mchana itakutana ili kujadili masuala ya kiusalama ikiwamo ya kuuawa kwa polisi na raia nchini.
Spika wa Bunge, Job Ndugai ameyasema hay oleo baada ya kipindi cha maswali na majibu alipokuwa akijibu muongozo wa Mbunge wa Bukombe, (CCM) Dotto Bitteko.
Polisi wanane waliuawa na watu wanaodaiwa kuwa majambazi, wilayani Kibiti, mwishoni mwa wiki iliyopita.