-->

Kanumba Kafa na Sanaa Imekufa – Steve Nyerere

Muigizaji wa Filamu Steve Nyerere amefunguka ya moyoni kuhusu kifo cha marehemu Steven Kanumba na kufa kwa tasnia ya filamu nchini, ambayo wasanii wengi wamekuwa wakipinga kauli hiyo.

Steven-Kanumba-pics

Katika ukurasa wake wa instagram Steve Nyerere amepost picha ya marehemu Steven Kanumba akikumbuka kifo chake na kuandika ujumbe akisema kuwa muigizaji huyo nguli, ameondoka na sanaa ya filamu na kilichobaki kwa wasanii ni chuki na unafiki.

“Tukatae tubishe king kaondoka na Sanaa yake, sasa ivi nipo chuki kuchekeana kichina, so sijaona mwana harakati kama Kanumba anayeweza kuthubutu kwenye mambo mbalimbali ya sanaaa. Wengi wameridhika na hela ya mboga gari basi, sio kutanua soko kuwa la kimataifa. Kanumba aliitangaza tasnia ndani na nje, Kanumba Kanumba Kanumba Kanumba, du sitaki sema meengii pumzika mzaziiiiiiii, da ngumu kuwa mbali nawe lakini kila jambo anapanga Mungu, uku mambo yale yale amna mabadiliko ukiwa na wenzako mmekaa usiache chakula kwenda msalani ama soda ohooooooooooo itakula kwako”, Aliandika Steve Nyerere.

Tarehe kama ya leo 7/4/2012 Steven Kanumbba alifariki dunia akiwa nyumbani kwake Sinza jijini Dar es salaam, baada ya kuteleza na kuangukia kichwa, kilichosababisha kupata brain concusion.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364