-->

Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu atoa neno kwa wasanii wa filamu nchini

Wasanii wa filamu nchini wametakiwa kuzingatia maadili na nidhamu ili waweze kufanikiwa katika kazi zao.

Rai hiyo imetolea na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fissoo alipokuwa akiwasilisha mada katika kikao kazi cha maafisa Utamaduni na wadau wa tasnia ya filamu wa mkoa wa Arusha iliyofanyika jana Jijini Arusha.

Mama Fissoo alisema kuwa nidhamu imekuwa kikwazo kikubwa kwa wasanii jambo linalowafanya wasiaminike miongoni mwa jamii ikiwa ni pamoja na taasisi za kifedha ambazo zingeweza kuwawezesha.

“Mnapaswa kuwa na nidhamu ya hali ya juu, wasanii wengi hasa wa tasnia ya filamu mmeshindwa kuaminiwa kutokana na nidhamu inayotiliwa mashaka,” alisisitiza Mama Fissoo.

Kwa upande wake Katibu Umoja wa Wasanii wa Filamu Mkoa wa Arusha, Said Mohamed Gogola ameishukuru Serikali kupitia Bodi ya Filamu kwa kuona umuhimu wa kukutana na wadau wa tasnia hiyo ili kuwajengea uelewa juu ya mambo mbalimbali yanayohusiana na maendeleo ya tasnia hiyo.

Amesema kuwa kikao kazi hicho kimewapa chachu ya kupiga hatua mbele zaidi katika kuhakikisha tasnia ya filamu mkoani Arusha inasonga mbele kwa kasi zaidi.

Naye Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Hargeney Chitukuro ameishukuru Bodi ya Filamu kwa kuupa mkoa wao fursa ya kukutanisha wadau wa tasnia hiyo na kuongeza kuwa wao kama Serikali ya Mkoa wako tayari kutoa ushirikiano ili kuhakikisha vijana wa mkoa wa Arusha wanapata ajira ya uhakika kupitia filamu.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364