-->

Wolper: Sijawahi Kuumia Kuachana na Mpenzi

STAA wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper amefunguka kuwa licha ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume tofauti na kubwagana nao, kamwe hajawahi kuumia kuachana nao.

Akichonga na Showbiz Xtra, Wolper alisema alikuwa na kawaida ya kuwaanika wanaume aliokuwa akiingia nao kwenye uhusiano ili watu wote wajue akidhani itakuwa ngumu kusalitiwa lakini ikawa kinyume chake na kuachana nao jambo ambalo hajawahi kujutia au kuumia kwa kuwa akiachana na mtu anaangalia waliopo kwenye foleni anachangua tu anayemtaka.

“Sijawahi kuumia kuachana na mwanaume ila kinachoniumiza sana ni kwa nini nilimtangaza watu wakamjua ndiyo maana kwa sasa sitaki tena kumtangaza niliyenaye, siwezi kuumizwa na kuachana kwa kuwa unakuta wengi wako kwenye foleni naangalia mwenye sifa za kuwa nami sichagui ana kazi au fedha naangalia mwenye mapenzi,” alisema Wolper.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364