Kauli ya Idris baada ya Wema Sepetu kuzingua
Katika uzinduzi wa viatu vya ‘SultanXforemen’, mchekeshaji Idris Sultan ametaja sababu ya mrembo Wema Sepetu kutofika katika uzinduzi huo.
Akiongea na Bongo5, Idris amesema alimualika mrembo huyo ambaye alikuwa date wake katika uzinduzi wa filamu ya ‘Heaven Sent’ wikiendi iliyopita na ila mrembo huyo hajafika kutokana na udhuru aliyopata hivyo akampa ridhaa.
“Nilimualika Wema sema unajua nyie wanawake mambo yenu hivyo ameshindwa kuja ikabidi ni mpe ridhaa, wakati naongea naye kwenye simu alivyosema sitaweza kufika basi nikamjibu uliza kiatu,” amesema Idris.
Idris na Wema wamekuwa wkionekana mara kadhaa katika event mbalimbali ,hivyo kukosekana kwa mrembo huyo kuliibua maswali kadhaa jambo ambalo Idis alinyoosha maelezo.