Wakunizima Hajazaliwa -Wema Sepetu
Malkia wa filamu Bongo , Wema Abraham Sepetu ametupa jiwe gizani ambalo bado halijajulikana ni kwenda kwa mtu gani na kumwambia bado wa kumshusha hajazaliwa kwani yeye alivyo ni majaaliwa kutoka kwa maulana na siyo kujitakia.
Wema ametupa jiwe hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram na kusema kuna mtu kamuharibia siku hivyo na kumwambia kwamba yeye hakujitakia kuwa alivyo hivyo mtu huyo ajue kutofautisha.
“Wa kunizima hajazaliwa bado jamani… Alafu mjue kutofautisha kati ya Kujaaliwa na kujitakia… Alhamdulillah nyingi kwa Maulana wangu… Sikujitakia… Ni majaaliwa tu… To whom it may Concern… Kuna mtu kajua kuniharibia siku wallah… ” Wema Sepetu.