-->

Video: Baada ya Tupac Chid Benz amvuta Jay Z

Baada ya sakata la kusema amefanya collabo na Tupac na kuleta mtafaruku mkubwa kwa mashabiki huku wakimtolea maneno makali wakisema amesha athirika kiakili kwa madawa ya kulevya kwa kuwa Tupac ni marehemu, sasa Chid Benz kuja na collabo na Jay Z.

Akifanya mahojiano kwenye kipindi cha Friday Night Live kinachorushwa na East Africa Television and Radio, Chid Benz amesema Collabo hiyo ameifanya na Jay Z huku ‘chorus’ yake ikifanywa na mke wa msanii hyo Beyonce, lakini anataka atoe ‘chorus’ hiyo na amuweke msanii wa Bongo Linah Sanga.

Chid Benz aliendelea kusema kuwa kauli hiyo anaitoa akiwa yuko sawa na sio mtu aliyelewa na madawa ya kulevya, na kwamba collabo hiyo imeshafanyika na cd yake ipo nyumbani kwa mama yake ‘Mama Chid’.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364