-->

Kayumba Ataja Matumizi ya Milioni 50

Baada ya mshindi wa Bongo Star Search, Kayumba Juma kushinda kiasi cha pesa za kitanzania Milioni 50 bado ameonekana kukaa kwenye kambi ya Mkubwa na Wanawe.

KAYUMBA34

Stori zinazo endelea mtaani juu ya mshindi wa Bongo Star Search Kayumba Juma ni kuwa toka ashinde shindano hilo na kukabidhiwa milioni 50, bado anaishi kwa kufadhiliwa katika kituo cha Mkubwa na Wanawe.

E-newz ikataka kufahamu ukweli kuhusu unafuu wa maisha alioupata Kayumba baada ya ushindi wa milioni 50 na kwanini ameshindwa kupanga nyumba au kujenga.

Kayumba amejibu “Nimenunua kiwanja Mbagala na nipo kwenye ujenzi na muda si mrefu nitatoka katika kituo cha Mkubwa na Wanawe na nitawaonesha watu nyumba yangu ili waone kama sijachezea pesa nilizo shinda kama watu wengi wanavyodhani”.

Eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364