-->

Kiba na Diamond Kupatana Sasa Haiwezekani-Dully

Msanii mkongwe katika muziki wa Bongo fleva Dully Skyes ambaye kwa sasa anafanya vyema na wimbo wake ‘Inde’ amefunguka na kusema anauwezo wa kuwapatanisha wasanii Alikiba na Diamond na kumaliza tofauti zao

Japo anakiri wazi kuwa ugomvi wa wasanii hao kwa sasa ni mkubwa kwani umeshatoka mpka kwa watu wa nje.

Dully Skyes akiongea kwenye kipindi cha Planet bongo alisema kwa sasa wasanii hao kupatana ni jambo gumu sana ila yeye anasubiri mpka watakapotokea wasanii wengine wakubwa kama wao kwake itakuwa ni rahisi kuwaweka chini na kumaliza tofauti zao.

“Kuwapatanisha inawezekana lakini si kwa ‘Age’ hii waliyofikia ni ‘Age’ ya sifa kila mtu anataka sifa na kila mtu anataka kuwa mkubwa kwa hiyo mimi nitasubiri baadaye kidogo itakapofikia muda kama miaka mitano hivi mbele au mitatu Mungu akipenda, vuguvugu hili litakapokwisha mimi na uwezo wa kuwakutanisha na kuwaambia ugomvi umekwisha lakini kwa ugomvi wao kupata leo au kesho kwa sasa si kweli” alisema Dully Skyes

Dully Skyes alizidi kutoa ufafanuzi kwa nini wasanii hao kwa sasa kupatana si jambo rahisi na kusema ugomvi wao umetoka nje mpka kwa watu wao wa karibu na mpka kwa mashabiki hivyo inahitaji muda

“Unajua ugomvi wao si wa wao peke yao saizi ugomvi wao ni wa watu wengi kumbuka kuna team pale huyu ana team yake na huyu ana team yake, kwa hiyo kuanza kusimamisha watu kwanza wa nje wawe marafiki harafu kuja kuwakutanisha wenyewe, au uwakutanishe wao wawe marafiki harafu watu wa nje wawe marafiki ni kazi kubwa sana ngoja vuguvugu lao kwanza lipungue. Waje Alikiba na Diamond wengine harafu mimi nitaweza kuwatuliza wao” alimalizia Dully Skyes

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364