-->

Mashabiki Wananigombanisha na Gabo – Duma

Hivi karibuni kumekuwepo na maneno ya chini kwa chini kuwa washindani wawili waliokuwa kwenye kipengele kimoja katika tuzo kubwa zilizoteka Afrika Mashariki za EATV Gabo na Duma kuingia kwenye bifu zito baada ya Gabo kuchukua tuzo zote mbili.

Imekuwa kama desturi kila baada ya tuzo fulani kutolewa kuibuka maneno mbalimbali kutoka kwa washindani au mashabiki,

eNewz ya EATV imezungumza na Duma na amesema kuwa yeye hajakasirika wala hana bifu na Gabo na hata kuna baadhi ya mashabiki ambao walitaka kuwagombanisha lakini wote wanajua nini wanachokifanya na pia alipost katika mitandao ya kijamii na kumpongeza msanii huyo pamoja na wengine walioshinda hiyo yote ni kuonesha kuwa hana tatizo na msanii huyo.

“Mimi na Gabo ni washkaji na sina bifu lolote na tuzo zimetupa changamoto sana na mimi nahisi ni msanii pekee ambaye nilimpost Gabo na wasanii wote waliopata tuzo, EATV haiwajachagua mtu bali watu ndio wamechagua mshindi ni nani hivyo sina tatizo lolote na Gabo.”

Pia amemaliza kwa kusema kuwa yuko mbioni kutoa kazi nyingine ya filamu mwakani kwa hiyo mashabiki wakae mkao wa kula na kusubiri filamu.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364