-->

‘Kiboko Kabisa’ ya Nisha Inahesabu Siku

KIBOKO KABISA

ILE Filamu ya Kiboko Kabisa kutoka kwa gwiji la Uchekeshaji Swahilihood Salma Jabu ‘Nishabebee’ ipo tayari na inehesabu siku kadhaa ili iruke mtaani na kufanya fujo za hatari huko kunako soko ni kazi safi si ya kuikosa kwani imejaa mastaa kibao.

Akiongea na FC Production meneja wa Nisha’s Film Productions Othuman Ochu amesema kuwa kila kitu kipo tayari ikiwa printing na mzigo umekamilika kwa ajili ya kuingia sokoni tarehe 29.January. 2016 na itapatikana nchi nzima katika maduka ya filamu za Kibongo.

“Filamu ya Kiboko Kabisa imekamilika na ipo kwa ajili ya kuingia sokoni soon na inakuja kuwashika sokoni wale wote waliingiza kazi zao sokoni ni kazi nzuri nay a kipekee kabisa kutengenezwa Bongo,”anasema Ochu.

Sinema ya Kiboko kabisa imetengenezwa na kampuni ya Nisha’s Film productions huku ikiwa imewashirikisha wasanii nyota wanaotamba sokoni kama vile King Majuto, Ben Blanco, Mzee Jengua, Nishabebee na wasanii wakali katika tasnia ya filamu Bongo si ya kuikosa.

FC

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364