-->

Makala: Kifo Bongo Movie, Mazishi Bongo Fleva, Kaburi ni Media

Kutoka Instagram, muigizaji mkongwe Norah ameandika.

Norah

Ni kama Chid Benz. Tofauti yake ni kwamba tasnia ya filamu haijapelekwa ‘soba hausi’. Wasanii na wadau wa filamu wamechoka. Wameishiwa mbinu. Nguvu. Na mizuka ya kazi.
Sanaa imegeuka kijiwe cha watu wasio na malengo na maisha. Wanajifanyia tu.

Ndicho kilichoifikisha hapa tasnia hii yenye mamilioni ya mashabiki na pesa.
Soko la filamu Bongo liko mahututi. Wafanyabiashara mitaani wako hoi. Mashabiki wako taabani.. Na wasanii wenyewe wako ‘mochwari’. Kuna jambo la makusudi linatakiwa kufanywa katika hili. Wasanii wanatakiwa kujitoa kwa dhati kutumikia vipaji vyao.
Na ili kufanya mambo yawe bora zaidi, wadau wa filamu wanatakiwa wajitoee kwa dhati kusukuma soko la filamu.

Ni ajabu kuendelea kuwaza kuwa sura ya Jackline Wolper itauza filamu kuliko kipaji cha Monalisa.
Ni ujinga kuendelea kuwaza kuwa nguo fupi za kikahaba zitafanya soko kuwa maarufu kuliko ubora wa stori.

Walewale ambao juzi tu walifanya vijana wengi washawishike kuingia katika uigizaji. Leo nao wana ndoto ya kuwa wanamuziki.
Kinachoshangaza wanaingia kwenye muziki kwa namna ile ile ya ‘kiki’ za filamu. Shilole alisema yuko mbioni kutoa wimbo na J. Lo. Kwa wenye akili taa nyekundu ziliwaka kichwani.
Tukajua yale yale. Mpaka leo hatujajua ni J. Lo yupi. Yule aliyemzalia Mc Anthony watoto mapacha au J.LO wa Kipare aliyezaa na Mganda, ‘Sintah’? Kuangalia zaidi sura na shepu badala ya vipaji halisi. Wamefanya sanaa ya filamu ionekane kitu chepesi sana. Gonjwa hilo limehamia kwenye muziki. Kila msichana mwenye sura na umbo zuri. Anaamini kuja kuwa bora zaidi ya Lady Jaydee.

Na bahati mbaya mitandao ya kijamii imejenga urafikii nao. Wanapewa ‘sapoti’ na kujikuta wakipata mashabiki ‘mitandao’. Mitandao ya kijamii kwa sasa ina nguvu kuliko wauza unga. Inaweza kukuhamisha mjini. Kukupora cheo. Kukupa mke. Kuvunja ndoa. Kukutajirisha. Kukufilisi. Mitandao ni zaidi ya ugaidi.

Na Wabongo wanapenda vitu vyepesi. Hawapendi vitu vya kufikirisha sana.
Na kirusi hiki kimesambaa kwenye vyumba vya wamiliki na wafanyakazi wa vyombo vya habari. Nao wameingia mkenge huu.
Kuamini kuwa wenye muonekano na sura nzuri

By Nora

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364