VIDEO:Mzee Hashim Rungwe Autaka Ukocha wa Taifa Stars
Mwenendo usioridhisha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, umemuibua Mwenyekiti wa chama cha siasa cha Ukombozi wa Umma, (CHAUMMA), Mzee Hashim Rungwe, kutaka yeye ndiyo aitwe kuwa kocha wa timu hiyo.
Mzee Rungwe ambaye alikuwa KIKAANGONI ya EATV, alikutana na swali lililomkumbusha wakati alipowahi kutamka kuwa anahitaji kuwa kocha wa timu, ambapo mzee Rungwe amekiri na kusisitiza kuwa bado anaihitaji nafasi hiyo hata sasa.
“Mimi nina uzoefu, nimecheza mpira, mimi ni mtu wa mpira, kama makocha hawa wanazembea, waniweke mimi, kwani nashindwa nini?” Amesema Rungwe
Pia ameweka wazi kuwa yeye ni shabiki mkubwa wa Simba tangu enzi za Sunderland na kwamba yuko tayari pia kuifundisha hata Simba.
Alipoulizwa kuwa ni kwanini asitume maombi yake TFF, amesema “Siwezi kuomba, umri wangu hapaswi kuomba, mimi mtu mzima, wanatakiwa wanifuate, waniite tu, mimi nitakwenda”
Katika hatua nyingine amesema tatizo la njaa ni sababu mojawapo inayofanya timu nyingi za Tanzania kushindwa kufanya vizuri kimataifa, ikiwemo Taifa Stars..
Huyu hapa Rungwe
eatv.tv