-->

Koko Byanko Afunguka Kumkamata Wema Sepetu

MWIGIZAJI wa Filamu Swahilihood anakuja juu katika uigizaji Koko Byanko ametamba kufanikiwa kuigiza na msanii nyota katika tasnia ya filamu Bongo Wema Sepetu ‘Madame Wema’ Koko amemshirikisha Wema katika sinema yake aliyoitengeneza hivi karibuni.

Wema-1

“Nilipo posti picha nikiwa na Wema wengi walinituhumu kama natoka naye lakini ukweli sitoki naye bali zilikuwa ni picha tu za location nilizopiga naye katika filamu yangu huyu ni msanii mwenzangu tu,”

FC ilizipata picha hizo pamoja na msanii huyo kueleezea kuwa ni za filamu lakini zipo kiutata msanii huyo amedai kuwa kumpata Wema kushiriki filamu yake haikuwa rahisi kwani ilihitajika ushawishi mkubwa na gharama zake ni kubwa sana.

“Wema alipoiona script yangu ilivyo kali alikubali kuigiza katika filamu na ameigiza katika kiwango kikubwa sana nawaambia wapenzi wa sinema waisubiri kazi bora yenye mastaa kibao,”anasema Koko.

FC

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364