-->

Ali Kiba Kuwatambulisha Wasanii Ambao Wako Chini ya ‘Label’ Yake

Hivi unajua kama Ali Kiba aliwahi kuwasimamia wasanii kadhaa chini ya ‘label’ yake kama tunavyoona kwa baadhi ya wasanii wa hapa nchini kwa sasa,iliishia wapi ana mpango wa kurudi tena kusimamia wasanii.

kiba11

’Hivi vitu nilikuwa navyo muda mrefu ila havikuwa ‘promoted’unajua vitu vyangu vingi huwa vinakuwa kimyakimya nilikuwa na wasanii wengi lakini nilivyopumzika kufanya muziki kipindi kile ilibidi niwapumzishe kwasababu ya vitu ambavyo vilitokea nilichukua likizo, na sasa ili niweze kukaa sawa ndio lazima waweze nao kufanikiwa katika vitu vyao vya muziki, siwezi mimi nikawa nimepumzika halafu mashabiki wakawa wamenimis halafu nikamtoa msanii na watu wanielewa, hapana kiukweli lazima niwe vizuri na nikawaonyesha msanii wangu si unaona hadi sasa hivi nimerudi lakini mdogo wangu Abdul Kiba bado sijamleta lakini wapo wasanii wengi kama Dalila, na wengine ambao hawajasikika lakini kazi zao zipo studio, lakini kwasasa nipo vizuri ataanza Abdul na wengine watafuata’’ Alisema Ali Kiba.

 

Cloudsfm

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364