Kuigiza Ukahaba, Ulevi Si Dhambi- Dokii!
UMMY Wenceslaus ‘Dokii’ mwigizaji wa filamu wa kike mkongwe amefunguka kwa kusema kuwa msanii anapoigiza sehemu inayohusu ulevi au ukahaba haina maana ndio tabia yake halisi bali ni uhusika tu ambao ni njia mojawapo ya kuionyesha athari ya matukio hayo wala si tabia ya mhusika.
“Unapopewa nafasi ya kuigiza kama Kahaba au mlevi ukiangalia imani yako inakuwa ngumu lakini ukiangalia majukumu yanayokuzunguka, ni lazima uigize kwani una watoto wanahitaji ada, unatakiwa sadaka kuigiza nafasi hizo si dhambi,”alisema Dokii.
Doki analisema kuwa kuna wakati kuna watu wanaweza kuhoji kuwa Yule ameokoka lakini mbona anaigiza katika nafasi zile ambazo ni mbaya lakini wanasahau kuwa inawezekana ikawa ni sehemu ya uhubiri na hatupaswi kuwachukua walioanguka katika dhambi bali kuwaombea na kuwafundisha warudi njia katika sahihi.
Filamu Central