-->

Kumbe Tatizo ni Kanumba

KWA muda mrefu sasa kumekuwa na mijadala kwenye mitandao ya kijamii na hata katika vinywa vya mashabiki wa filamu za Kitanzania wakibishana kuhusu tasnia ya Bongo Movie, wapo wanaoamini imekufa na wengine kupinga jambo hilo.

Ray Kigosi na Marehemu Kanumba

Hata baadhi ya wasanii wa tasnia hiyo wenyewe wamegawanyika pia, kuna wanaamini ndio basi tena na wengine wakisema bado inaendelea kudunda ila, lipo tatizo na kuzinyooshea vidole kazi za nje kuwa ndio tatizo linalowakwaza.

Ndio maana haikushangaza hivi karibuni, baadhi ya wasanii walifikia hatua ya kuandamana katika barabara kadhaa za jijini Dar es Salaam kuonyesha msimamo wao wa kupinga kazi za nje wakiamini ndizo zinazoua soko la kazi zao.

Mwanaspoti ambalo ni miongoni mwa wadau wakubwa wa tasnia hiyo, liliamua kumfungia safari mmoja ya nyota wa filamu Tanzania ambaye enzi za uhai wa Steven Kanumba walikuwa wakichuana na kufanya soko la tasnia hiyo kusimama imara kwelikweli.

Vincent Kigosi ‘Ray’ ndiye aliyezukiwa maskani kwake jijini Dar es Salaam na kufanyiwa mahojiano maalumu juu ya ukweli uliopo kuhusiana na kuporomoka kwa soko la filamu Tanzania na kutaka kujua kama ni kweli ndio limekufa ama la.

Jamaa wala hakuvuga kitu, aliamua kufunguka ukweli kwa mtazamo wake, tatizo ni nini na kitu gani kifanyike, mbali na kuzama kwenye historia ya maisha yake kwa ujumla kuanzia sanaa hadi ya kawaida na mipango yake. Hebu endelea naye….!

JAMAA MBISHI KINOMA

Ray ambaye alikuwa gumzo hivi karibuni kutokana na utani wake juu ya kudai weupe wake umetokana na kunywa maji mengi, kwanza anakataa kuwa sanaa ya filamu imekufa kama baadhi ya watu wanavyoamini.

Anasema tasnia hiyo haijafa, ila ni kweli imeyumba kutokana na hali ya maisha ilivyo na miundo mbinu inayochangia mambo kujitofautisha na miaka ya nyuma, ila anakiri soko kwa sasa halipo sawa.

“Tasnia ya filamu haijafa kama baadhi ya watu wanavyodai bali imeyumba na kuyumba ni kitu cha kawaida kabisa kwa binadamu kwani anaweza kuanguka na akasimama tena,” anasema.

Anasema kwa hali hiyo wao kama watayarishaji wakubwa wamekaa kimya wakijipanga na kuendeleza harakati ambazo zitainua tena soko lao na filamu kurudi katika ubora wao kama zamani pamoja na changamoto zinazojitokeza kwao ni kipindi cha mpito tu.

“Lazima tasnia itarudi kama awali, ni sawa tu na maisha ya mtu asiyekata tamaa katika kutafuta anapopata changamoto anajipanga na kurudi tena na sisi itakuwa hivyo tutarudi kama awali,” anasema.

Mwanaspoti

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364