-->

Kuvaa Nusu Utupu Natangaza Brand- Vanessa Mdee

Msanii wa muziki wa bogno fleva ambaye anafanya poa katika anga za kimataifa Vanesa mdee, amefunguka sababu ya yeye kupenda kuvaa nguo za nusu utupu.

Vanessa-Mdee

Akiwa kwenye kipindi cha Friday Night Live kinachorushwa na East Africa Radio na EATV, Vanessa Mdee amesema anapenda kuvaa mavazi hayo ambayo hayakubaliki kwa jamii, kwa sababu anatangaza brand yake, na hatimaye impe dili la matangazo kwa wabunifu wa mavazi.

“Ukweli ni huu, wasanii for a long time in the past, wasanii wa kitanzania hawajajua na kutambua brand yao, mi brand yangu mi nataka ndani ya miaka miwili napigiwa simu na Balmain, na Lui V, nataka dersigners wakubwa wa dunia wanitumie kutangaza bidhaa yao kwa sababu wanaamini nina brand yangu kubwa na zinaendana, so nna malengo , na if im gonna offend any body im sory”, alisema Vanessa Mdee.

Vanessa Mdee ambaye kwa sasa ameachia video yake mpya ya Kaniroge, amesema ana mipnago ya kufika na kutambulika dunia nzima katika kazi zake za muziki, kama alivyochora ramani ya dunia kwenye mkono wake.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364