-->

Lady Jaydee Kula na Mashabiki Wake

MKALI wa wimbo wa ‘Ndi ndi ndi’, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’, ameonyesha kuwateka mashabiki wake kwa kuchagua video tatu nzuri wanazomtumia kisha anakwenda kula nao chakula cha jioni na kuwa nao katika matukio yake makubwa ya kimuziki.

JIDEE

Katika maelezo yake aliyoweka katika ukurasa wake wa facebook, Jay Dee aliandika kwamba waliomtumia video wakiwa wanaimba wimbo wa ‘Ndi ndi ndi’ atachagua majina matatu ya walioburudisha vema zaidi kisha atawataja siku zijazo kwa ajili ya chakula hicho.

“Nitachagua ‘Clips 3’ bora zilizokonga na kusuuza watu wengi na watatu hao nitafanya mchakato wa kula nao japo ‘dinner’ pamoja na ‘ku-hang’ nao siku yoyote nikiwa na ‘event’ kubwa, majina nitataja baadaye kidogo,’’ aliandika Jay Dee.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364