Lazima Wawepo Wabaya wako Ili Uwajue Wazuri Wako….-Lulu
Lazima Giza Liwepo Usiku na mwanga uwepo Mchana Ili tuweze kutofautisha Usiku Na Mchana
Lazima wawepo Wanaokuchukia Ili uweze kuwajua wanaokupenda?
Lazima Wawepo Wabaya wako Ili uwajue Wazuri wako….maana bila hao Wabaya hutoweza kutofautisha yupi ni yupi.
Sio kwa watu tu hii ina apply kwenye vitu vingi tu tofauti..!
Ili uweze kujua Positive Side ya Kitu Lazima kuwe na Negative Side yake Pia..!
Ninachojaribu kusema ni kwamba Kila mtu ana Umuhimu wake na nafasi yake katika Maisha yako(Na kila kitu pia)…Unachotakiwa ni kujifunza kupitia Aina tofauti ya watu unaozungukwa nao au Vitu unavyozungukwa navyo…don’t ever force negative iwe positive au positive iwe negative….ipo sababu ya hicho kitu au mtu kuwa jinsi kilivyo..!
Jumapili njema..!❤️
@elizabethmichaelofficial on instagram