-->

Si Mchina ni Umbo Langu – Sasha

MWIGIZAJI chipukizi katika tasnia ya filamu Bongo Sophia Salim ‘Sasha’ mwenye umbo la Kibantu amesema kuwa ni umbile lake na hajui wala hajawahi kutumia dawa za Kichina kama vile ambavyo wengine wanadaiwa kufanya kitu hicho yeye amezaliwa hivyo na anajivunia kuwa hivyo.

Sophia Salim ‘Sasha’

“Jamani hili ni umbo langu halisi nimeumbwa hivi na sijawahi wala sijui hizo habari za mchina sijatumia dawa yoyote niwe hivi kuna watu wanajinufaisha kwa kutumia picha zangu?,”alisema Sasha.

“Kuna watu ambao wanatumia picha zangu katika matangazo ya kukuza makalio Napata usumbufu sana kwa kupigiwa simu kama dawa hizi hazina madhara,”

Sasha ambaye ni mwigizaji mpya kabisa akishiriki katika tamthilia ya Siri za familia anasema kuwa baadhi ya watu wanaouuza dawa za shepu wamekuwa wakitumia picha zake wakiwadanganya watu kuwa wakitumia dawa zao watakuwa na shepu kama yake, anasema wasiwaamini yeye hajatumia dawa.

Sasha akiwa kwenye moja ya kipande cha tamthilia ya siri za familia

Tamthilia ya Siri za familia season four inazidi kujikita kwa wapenzi na kutengeneza watazamaji wapya kila siku na kuwaleta wasanii nyota ambao wamekuwa ni kivutio sana kwao tamthilia hiyo uruka kila siku kuanzia jumatatu hadi Ijumaa kupitia runinga ya East Africa tv.

Filamucentral

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364