-->

Lissu Afutiwa Mashataka, Akamatwa Tena

Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu amekamatwa na polisi katika mahakama ya Kisutu wakati akitoka kuhudhuria kesi yake ya uchochezi.

Tundu Lissu

Taarifa ya kukamatwa lwa Lissu imethibitishwa na Afisa Habari wa chama hicho, Tumaini Makene, ambaye amesema kuwa Lissu amekamatwa bila kupewa maelezo yoyote ya sababu za kukamatwa kwake, na amepelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam..

Kupitia mitandao ya kijamii, Lissu ameandika….

“Nimekamatiwa mahakamani Kisutu mara tu baada ya waendesha mashtaka wa serikali hii kunifutia kesi iliyotokana na kukamatwa kwangu bungeni Dodoma mwezi uliopita.

Hiyo kesi wameifuta kwa maelezo kwamba serikali haina nia tena ya kuendelea na kesi hiyo. Sikutoka hata nje ya mahakama nikakamatwa tena. Wamenileta Central kwa mahojiano.

Mapolisi walionikamata wamekataa kuniambia wananikamata kwa kosa gani. Kwa hiyo sijui kosa nilofanya hadi sasa. Nadhani sababu ina uhusiano wa moja kwa moja Uchaguzi wa Rais wa TLS unaofanyika wiki ijayo.”

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364