-->

Lulu Afunguka Juu ya Alikiba na Ommy Dimpoz

Msanii wa filamu nchini Lulu Michael ambaye wiki hii alikuwa akitangaza kipindi cha ‘NgazKwaNgaz’ alifunguka na kuweka wazi kuwa msanii Ommy Dimpoz na Alikiba ni watu ambao wamekuwa wakifanya vizuri kila wanapokutana.

Lulu Michael alidai kuwa wakali hao wa bongo fleva wamekuwa wakifanya vyema kila walipokutana na kutengeneza kazi nzuri ambazo zinapendwa na watu.

 

“Katika Top 20 zangu mwaka 2016 zilizonifurahisha sana kazi ya Alikiba na Ommy Dimpoz inakuwa namba 4, yaani Ommy Dimpoz akikaa na Alikiba wanafanya kitu kizuri, ile verse ya Alikiba kwenye Kajiandae ni tamu sana unaweza kuinywea chai bila hata andazi. Sijui sasa Alikiba ndiyo mjanja wa Ommy Dimpoz? Maana nakumbuka hata ule wimbo wao wa kwanza ‘Nai nai’ ulifanya vizuri sanaa” alisema Lulu Michael

Mbali na hilo Lulu Michael anasema sababu kubwa kuipenda video ya ‘Kajiandae’ kwanza namna wasanii pamoja na dancers walivyoweza kuvaa vizuri, lakini pia mwanamke aliyetumika kama video queen alikuwa na muonekano mzuri wenye kuvutia na kuleta utofauti.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364