-->

Martin Kadinda: Wema Amebadilika Hadi Raha

ALIYEKUWA Meneja wa Mrembo wa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, Martin Kadinda, amempongeza mwanadada huyo kwa kubadilisha mfumo wa maisha yake.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Martin alisema kitendo cha Wema kufuta picha zake kwenye mitandao ya kijamii na kubadili tabia za kuweka wazi maisha yake ni hatua ya kupongezwa.

“Uamuzi alioufanya Wema ni hatua nzuri na ya kupongezwa, mimi na familia yake hatukuwa tukipendezwa nayo kwa kuwa ilikuwa ikichafua jina lake,” alieleza Martin.

Martin aliongeza kwamba Wema ambaye amebadili meneja kwa sasa, amekuwa tofauti na alivyozoeleka maana amekuwa muelewa na msikivu kwa anachoelekezwa.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364