Lulu Afunguka, Mama Kanumba Ajibu
STAA wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ anadaiwa kulinogesha bifu lake na mama wa aliyekuwa nguli wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegeo kufuatia posti yake ya hivi karibuni akiashiria kumtisha mama huyo.
Lulu juzikati alitupia ujumbe mtandaoni akimjibu mmoja wa mashabiki wake aliyeuliza sababu ya yeye na mama Kanumba kutoiva ambapo aliandika:
“…ni hivi mimi siyo chizi jamani kila ninachokifanya nakijua vizuri tu, mimi ndo’ najua ‘what’s going inside’ (nini kinachoendelea) nyinyi wa nje yasikieni hivyohivyo, sitajibu watu wala mhusika mwenyewe ila siku ikifika nitaongea.”
Baada ya kupostiwa kwa ujumbe huo, mashabiki walimjia juu Lulu wakieleza kuwa, hana sababu ya kumtisha mama Kanumba badala yake kama kuna lililo moyoni mwake aliseme kuliko kukaa kimya.
“Huku sasa ni kumtisha mama wa watu, kama analo jambo aliseme watu wajue sababu ya bifu lao,” alisema mmoja wa mashabiki.
Baada ya kulipata hilo paparazi wetu alimtafuta mama Kanumba na kumuuliza juu ya maneno hayo yaliyotafsiriwa kuwa ni ya vitisho kwake ambapo alifunguka:
“Namshangaa sana huyu mtoto, ana siri gani nzito baina yangu mimi na yeye, sina siri naye huenda anataka kutoa siri ya kifo cha mwanangu aitoe basi, tena aitoe haraka hiyo siri wala asisubiri hiyo siku ifike.
“Tena itakuwa vizuri akiita vyombo vya habari na kuianika kama ni kubwa hivyo au aniite aniambie, nimemuacha na maisha yake ananifuatafuata sitaki kabisa.”
Kwa upande wake Lulu alipotafutwa kuzungumzia ishu hiyo alijibu kwa kifupi; “Nimeshasema sitaki kuongea na mtu yeyote kwa sasa, tena wewe mwandishi ‘nimeshaku-block’ nashangaa unanipigia kwa namba nyingine.”
Chanzo:GPL