Odama Kuanza Mwaka na Filamu ya Mkwe
Staa wa Bongo Movie, Jeniffer Kyaka maarufu kama Odama anakuja na movie yake mpya ya ‘Mkwe’.
Odama ni miongoni kati ya wasanii wenye vipaji vya kuigiza kwenye kiwanda cha Bongo Movie. Mpaka sasa amefanikiwa kufungua kampuni yake ya production (J Film For Life) ambayo tayari ameshafanikiwa kupata deals kadhaa.
Tarehe 25 ya mwezi huu wa nne, Odama ataachia filamu yake mpya ya ‘Mkwe’ ambamo ndani yake wameshiriki mastaa wenye uwezo mkubwa kama Odama mwenyewe, Hemedy PHD, Lilian Iwey na wengine wengi.