Lulu Awajibu Wanaomnanga Mtandaoni
MTOTO mzuri Bongo Muvi, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amewataka wanaomsema kuwa ni mfupi, wampime kwa akili zake maana yeye harefuki mwili lakini anarefuka akili.
Akizungumzia ufupi huo ambao umekuwa ukijadiliwa mara kwa mara mitandaoni, Lulu alisema anaufunga mjadala huo kwa kuwataka wanaomjadili wafuatilie matendo yanayofanywa na uwezo wa akili yake.
“Niwaulize tu wanamuoanaje Lulu wa miaka ile na Lulu wa sasa? Mimi sina haja ya kukua umbo halafu akili ikawa ndogo, nakua kiakili hivyo hata nikiwa na umbo hilihili miaka yote sioni tatizo,” alisema Lulu.
Chanzo:GPL