-->

Lulu, Gigy Money Wacharuana

MASTAA wawili wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Gift Stanford ‘Gigy Money’ wamejikuta wakiingia kwenye mtifuano mkali baada ya kutoleana maneno machafu.

GIGY89

Chanzo makini kilieleza kuwa ishu ilianzia kwa Gigy ambaye alisema mwanadada Lulu hajui kuvaa anavaa matangazo, hii ni baada ya kuulizwa na kituo kimoja cha runinga kwamba ataje mastaa kumi wanaojua kuvaa ambapo Lulu alimjibu kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa Instagram kuwa bora asijue kuvaa lakini hawezi kuvaa matambara kama yeye.

“Yaani Gigy alikasirishwa sana na kitendo cha Lulu kumwambia anavaa matambara alijikuta akipaniki na yeye akaendelea kushilikilia msimamo kwamba anavaa nguo za matangazo hivyo ni bora yeye anayevaa matambara anayonunua mwenyewe kuliko yeye,” kilisema chanzo.

Baada ya kupata maelezo ya chanzo, paparazi wetu alimtafuta Gigy na kumuuliza kulikoni ambapo alisema amekasirishwa sana na kitendo cha Lulu kumwambia anavaa matambara wakati yeye alizungumza kama anavyoona kwani mavazi anayovaa hayaendani na mazingira.

“Matambara ni ya kwangu na haya ni maisha yangu siyo yeye anayevaa nguo za matangazo eti anajiona naye anavaa maana naona Lulu ameunda na kampeni na makundi kwa ajili ya kunishambulia, mimi ni jeshi la mtu mmoja hawaniwezi,” alisema Gigy Money.

Ili kuleta mzani wa habari, gazeti hili lilimtafuta Lulu lakini mpaka linaenda mtamboni simu yake ilikuwa ikiita tu bila kupokelewa.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364