-->

Kuelekea Ramadhan, Nisha Afanya Jambo Hili

 

nisha-4

ZIKIWA zimesalia siku chache kabla ya mwezi mtukufu wa Ramadhan kuanza, staa wa filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ jana aliukaribisha kwa kula chakula cha jioni na watoto yatima.

Nisha aliwatembelea watoto yatima wa kituo cha New Hope Family Group kilichopo Kigamboni, Dar,  ambapo alipata nafasi ya kula nao chakula cha jioni alichokiandalia, hali iliyosababisha watoto hao kufurahia vilivyo.

Akizungumza kituoni hapo, Nisha alisema ameamua kushiriki na watoto hao chakula hicho ili kuukaribisha mwezi mtukufu kwani atasafiri nje ya nchi hivyo akaona ni vyema kuwaachia japo msaada wa chakula na mahitaji mengine.

“Nawapenda sana watoto yatima na kila mwisho wa mwezi huwa nakuja kuwaona, mwisho wa mwezi huu mpaka Ramadhan inaanza sitakuwepo ndiyo maana nimekuja leo,” alisema Nisha.

nisha-5 nisha-3 nisha-2 nisha-1

 

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364