-->

Lulu: Tuzo Hii ni Mpango wa Mungu, Kutokana na Matatizo Niliyopitia Maishani

Mshindi wa tuzo ya Best Movie-East Africa, Elizabeth Michael ‘Lulu’ alieleza hayo mara tu baada ya kutua Dar-es-salaam akitokea Lagos Nigeria na tuzo yake.

LULU321145
‘’Kila kitu ambacho kinatokea sasa hivi nakiweka ‘in a way’ zaidi ya mpango wa Mwenyezi Mungu nisingepitia ambavyo nimepitia katika maisha yangu nisingeenda Africa Magic ,ningekuwa labda nimeshakufa au nimeshaacha kuigiza labda nisingekuwa na moyo huu wa kuendelea kukomaa,matatizo niliyopitia ndio yamenifanya niwe na moyo wa kuwa kuendelea kufanya kazi na kuwadhibitishia watu kuwa walichokuwa wakikifikiria kwangu ni tofauti’’Alisema Lulu.

‘’Mungu ameweka kitu hiki ndani yangu,’problem’ ningekuwa na ‘flat life’ ningezoeleka kama msanii wa kawaida nacheza movie moja naacha nacheza ya pili,ya tatu naacha,nadhani hii njia yangu ambayo Mungu alikuwa amenitengenezea na sijui pengine nina mengi kiasi gani mbele ambayo ninakutana nayo’’Aliongeza Lulu.

Cloudsfm.com

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364