Lupita: Malengo Yangu Hayajakamilika Bado
MKALI wa filamu nchini Marekani, Lupita Nyong’o, amedai kwamba japokuwa amepata mafanikio makubwa katika filamu, bado malengo yake hayajakamilika.
Msanii huyo alifanikiwa kutwaa tuzo za Oscar mwaka 2015, lakini amesisitiza kwamba lengo lake ni kuwa msanii mkubwa duniani kama ilivyo kwa wasanii wengine.
“Nimekuwa na mafanikio makubwa kutokana na filamu, lakini ninaamini bado malengo yangu hayajakamilika kwa kuwa ndoto zangu ni kufika kule ambako baadhi ya wasanii wa Marekani wamefikia.
“Ninaamini inawezekana kwa kuwa nilianza chini sana na sasa nimeweza kusogea, nitaendelea kujituma ili dunia initambue kama ilivyo kwa wasanii wakubwa wanaofanya vizuri duniani,” alisema Lupita.
Mtanzania