Madee amkataa Wolper kucheza video yake mpya
Msanii Madee Ali ‘Madee’ kutoka kundi la Tip Top Connection amefunguka kuwa anashangazwa na uvumi wa msanii mwenzake, Jackline Wolper kwa kudai kuwa ametumika katika video mpya ya msanii huyo ya ‘Sikila’ bila ruhusa yake.
“Ile video haijamuonyesha mtu sura zaidi ya kuwa na katuni hivyo nashangaa kusikia hivyo, kikubwa ni kuwa hajatumika yeye bali ametumika mwanamke mwingine kutoka Nigeria na anabidi aelewe ile sio picha bali ni mfano wa taswira tu,”alisema.
Akizungumzia mapokeo ya wimbo huo alisema kuwa mashabiki walishtuka kwasababu hawajawahi kuona kitu kama hicho kwa hapa nyumbani, lakini anashukuru Mungu mapokeo yamekuwa mazuri kwasababu wapo wanaosifia ubunifu na wapo wanaopinga ubunifu huo.
Mwananchi