-->

Napenda Kuwafunika kwa Pamba-Lulu

MWIGIZAJI, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka na kudai kuwa, hakuna kitu anachopenda kama kutupia viwalo na kwamba, kila kunapokuwa na hafla ni lazima avunje kabati.

Lulu alisema sio kwenye sherehe tu, bali hata katika kazi zake za filamu anapenda kutupia kwa sababu anapenda kuvaa na kuonekana tofauti kila mara ikiwa ni furaha yake.

“Mi napenda kupendeza kila wiki, kama nitatoka na kuwa sehemu iliyopendeza na nguo za kipekee kuna wakati nawatania rafiki zangu nikiwaambia waandae tu shughuli nije niwafunike kwa pamba kali,” alisema Lulu ambaye huko kwenye mitandao ya kijamii anasumbua sana kwa viwalo.

Hata hivyo, mwenyewe anasema kuwa mara nyingi akiona nguo nzuri huwa hajali sana kuhusu gharama kwani, inapobidi huibadilisha ili kuwa kama anavyoipenda.

Mbali na kupiga pamba, Lulu pia anapenda sana kujipodoa na ndio sababu hivi karibuni alitokelezea kama Rihanna.

Mwanaspoti

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364