Maisha Yaanza Kumnyokea Idris Sultan
Mshindi wa shindano la Big Brother 2014, Idris Sultan amesema ameanza kuingiza faida kutokana na uwekezaji aliyoufanya baada ya kutoka kwenye shindano la hilo ambalo lilimpatia zaidi ya Sh500 milioni.
Akizungumza na Bongo5, Idris alisema tayari ameanza kuona faida ya pesa ambazo aliwekeza kwenye biashara zake.
“Kwa sasa hivi matunda nimeanza yaona, kuna kipindi fulani nilikuwa sitoki sana, watu wakasema Idris amepotea kwa muda mrefu, hicho ndo kipindi ambacho nilikuwa busy kuweka mambo sawa, unajaribu kufanya hichi, unajaribu hichi ilimradi kuweka mambo sawa,” alisema Idris.
“Kwa hiyo sasa hivi ndiyo naona inshallah mambo yameanza kunyooka. Kazi zinaanza kutoa malipo ambayo yalitakiwa yatoke tangu zamani, lakini biashara zimechukua muda mrefu kidogo kutoa yale malipo ambayo yalikuwa yanastahili,”
Pia Idris amesema kwa sasa anafurahia kazi yake mpya ya utangazaji ambayo anafanya Choice FM.
Bongo5