-->

Majambazi 13 Wauawa Kibiti, Wakutwa na Bunduki 8 Pamoja na Pikipiki 2

Jeshi la Polisi Tanzania limesema wahalifu 13 wameuawa katika majibizano ya risasi katika eneo la Tangibovu lililopo katika kijiji cha Miwaleni Tarafa ya Kibiti mkoani Pwani ambapo polisi wamefanikiwa kukamata bunduki 8, pikipiki 2 na begi la nguo.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas kuhusiana na tukio la kuuawa wahalifu 13 katika majibizano ya risasi baina ya Polisi na wahalifu hao katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafaya Kibiti.

Jeshi la Polisi limeendeleza jitihada zake kuhakikisha mkoa wa Pwani na maeneo yake ya jirani yanakuwa salama na yenye amani kwa kuendelea kupambambana na wahalifu mbalimbali waliojificha mkoani humo  ambao wamekuwa wakifanya matukio mbalimbali ya kihalifu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa katika ziara mkoa wa Pwani mwezi Juni mwaka huu aliwataka wahalifu wote waliopo mkoani humo waache mara moja kufanya matukio ya kihalifu pia IGP Sirro aliwataka wahalifu kuacha mara moja kufanya uhalifu mkoani humo na kuwaambia kuwa mkono wa dola utawafikia kama wataendelea.

Mkoani Pwani zaidi wa watu 30 wameuawa na watu wasiojulikana kwa vipindi tofauti tofauti huku jeshi la polisi nalo likifanikisha kuwaua zaidi ya wahalifu 20 wanaodaiwa kuhusika na matukio mbalimbali ikiwepo yaliyokuwa yakifanyika mkoani humo na maeneo jirani.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364