-->

Majay Birthday: Lulu Amwambia Majay ‘I think Sisi ni Perfect Combo’

Leo ni siku ya kuzaliwa ya CEO wa EFM, Majay, ambapo wadau mbalimbali pamoja na watu wake wa karibu wanamtakia heri ya mafanikio katika maisha yake.

majay03

Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye anadaiwa kuwa kwenye mahusiano na bosi huyo, amekuwa ni mmoja kati wa watu waliomtumia ujumbe wa heri ya mafanikio huku ujumbe wake ukionyesha ukaribu wa kimahusiano zaidi.

“Juhudi zako, uchapakazi na ukarimu ni vitu vichache tu kati ya vingi ninavyojivunia na nakujifunza kutoka kwako, I think sisi ni perfect Combo,” aliandika Lulu instagram.

Aliongeza, “Nikiwa mkubwa nataka kuwa kama wewe bosi wangu (I mean kuwa CEO na vitu kama hivyo) Juhudi zako tunaziona, tuko nyuma yako na tunakuombea mafanikio zaidi na zaidi. Yesu Wangu akutunze kwa ajili yangu na familia yetu kwa ujumla. Happy birthday baba G, My successful,”

Tetesi za mahusiano ya Majay na Lulu zilishika kasi zaidi baada ya wawili hao kuongozana kwenda Nigeria katika utoaji wa Tuzo ya Africa Magic Viewers Choice (MVCA) 2016.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364