-->

Nilikunywa Pombe Kutoa Aibu Kwenye Video ya ‘Natafuta kiki’-Shilole

Msanii wa muziki wa bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amefunguka na kusema ilikuwa ni jambo gumu kwake kufanya video ya ‘Natafuta kiki’ ya msanii Raymond.

shilole-na-raymond

Msanii Raymond akiwa na Shilole wakati wa utengenezaji wa video ya ‘Natafuta kiki’

Amesema ugumu huo ni kutokana na ukweli kwamba ‘scene’ ambazo alipaswa kucheza zilikuwa ngumu kwake jambo ambalo lilimfanya atumie kwanza kilevi kuondoa aibu.
Shilole alisema hayo kupitia kipindi cha eNewz kinachorushwa na EATV na kudai alikuwa anashindwa kufanya mambo kwenye video hiyo kutokana na vile anavyomuheshimu Raymond kama mdogo wake.
“Mimi niliweka upendo na kuona nimsaidie mdogo wangu Raymond katika kazi yake ili iweze kutazamwa na watu wengi zaidi, ila kiukweli ilikuwa ni kazi mbaya sana kwangu na ngumu lakini nikaona maji nishayavulia nguo hivyo sina budi kuyaoga, nikamwambia Raymond wewe ni mdogo wangu sasa naanzaje kufanya haya mambo? Ilikuwa ni ngumu ikanibidi ninywe pombe kidogo ili niweze kuchangamka, kwani watu walikuwepo wengi nikawa naona aibu. Akaniambia hamna usijali hii kazi tu nisaidie tu, ikabidi nivae ile night dress na kuingia kazini” alisema Shilole.
Mbali na hilo Shilole alisema kuwa amekuwa akitumika kwenye baadhi ya video mbalimbali kutokana na wasanii hao kumuomba ashiriki kwenye video zao ili kuwasaidia video zao kuangaliwa na watu wengi zaidi.
“Nilifanya video ya Man Fongo haina ushemeji, video ya Darasa ‘Too much’ hii ya Raymond ‘Natafuta kiki’ na ile ya Dully Skyes na Harmonize ‘Inde’ wao wamekuwa wakiniomba na kusema uwepo wangu kwenye video zao unaleta ‘impact’ kwa watu kwani watu wanakuwa wanazitazama sana video zao hivyo mimi naamua kuwapa ‘support’.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364