-->

Majuto Awataka Wasanii Wafanye Haya

Majuto34

MCHEKESHAJI mkongwe nchini, Amri Athumani ‘King Majuto’, amefunguka na kudai kwamba kuna baadhi ya wasanii wa filamu wanafanya kazi zao bila ya kuwa na lengo la kuelimisha jamii zinazowazunguka.

Msanii huyo amedai kwamba, wasanii wengi wapo kwa ajili ya kufurahisha watu lakini wanasahau kwamba wanatakiwa kuelimisha jamii kwa kuwa wao ni kioo cha jamii.

“Ukiangalia filamu zangu nakuwa nachekesha lakini nafundisha, ila kuna wasanii wengine kazi yao kubwa ni kuchekesha katika kila filamu lakini hawatumii muda wao kwa ajili ya kuelimisha,” alisema Majuto.

Mkongwe huyo amekuwa na idadi kubwa ya mashabiki kutokana na uwezo wake wa uigizaji.

Mtanzania

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364