Man Fongo: BASATA Walitaka Kufungia Hainaga Ushemeji Nikawatuliza
Msanii wa muziki wa Singeli Man Fongo amesema aliitwa na Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) na kuhojiwa kuhusu maudhui ya wimbo wake ‘Hainaga Ushemeji’ ambao umeshafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.
Akiongea na Bongo5 wiki hii, Man Fongo amesema aliachiwa na baraza hilo baada ya kuonekana hana hatia.
“BASATA walinitafuta wakaniuliza vipi kijana mbona unapotosha? Nikawaambia sio kupotosha tunafanya muziki kulingana na wakati uliopo. Wakati huu unaweza ukawa na mpenzi wako lakini dakika mbili ukiondoka utakuta tayari rafiki yako au ndugu yako ameshachukua namba, kwa hiyo ni vitu vipo na vinatokea,” alisema Man Fongo.
Aliongeza, “So baada ya kuniuliza unapotosha nikawaambia sijapotosha, mimi nimeuliza nasikiaga hainaga ushemeji? vijana wakasema wanakula, kwahiyo ni kitu kipo na kinatokeaga, wakasema basi sawa kwa sababu umejitahidi kuimba kwa mafumbo,”