-->

Mzee Chilo Awataka Wasanii wa filamu Kubadili Mbinu

Nguli wa filamu, Ahmed Olotu maarufu kama ‘Mzee Chilo’ amesema anajua tasnia ya filamu inakumbwa na changamoto nyingi lakini wasanii wa filamu wanatakiwa kubadilisha mbinu za kibiasha ili wanufaike na kazi zao.

Mzee Chilo

Mzee Chilo

Akiongea na Bongo5 wiki hii, Chilo amewataka wasanii wa filamu kubadili mtazamo wa kibiashara ili waweze kunufaika na kazi zao.

“Mimi nasema tutengeneze kazi nzuri kama hali ni mbaya zaidi tubadili hata mbinu kwa tupeleka filamu zetu kwenye majumba ya sinema,” alisema Mzee Chilo. “Lakini tufanye kazi badala ya kulalamika. Tutapofanya kazi kwa bidii hata malalamiko yetu yatakuwa na uzito kwa sababu tunaweza tukawa tunalalamika halafu hatufanyi kazi kitu ambacho kinaweza kuwavunja moyo wale ambao wanataka kutusaidia,”

Pia muigizaji huyo ambaye ana miaka 10 ndani tasnia ya filamu, amesema mwaka 2016 ni mwaka ambao ameanza kuona mwanga wa mafanikio ukiongeza zaidi kwenye tasnia ya filamu.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364