-->

Masanja Mkandamizaji Awatembelea Majeruhi wa Lucky Vincent Marekani

Dar es Salaam. Msanii na Mhubiri wa Injili, Masanja Mkandamizaji leo amewatembelea wanafunzi majeruhi wa Shule ya Msingi ya Lucky Vincent nchini Marekani.

Masanja, aliyepata umaarufu katika kipindi cha televisheni cha ze comedy, ameandika katika ukurasa wake wa instagram akionyesha kumshukuru Mungu kwa kuwaona watoto hao akiwa Marekani.

“Mungu amenipa neema ya kwenda kuwaona wadogo zetu waliopata ajali, Sadia na Wilson na kuwepo Marekani kwa matibabu, imekuwa siku njema kwetu sote tumefurahi pamoja nao kula nao na kumtafakari Mungu kwa pamoja,” ameandika Masanja.

Wanafunzi hao walipata ajali ya gari wilayani Mbulu, mnamo Mei mwaka huu wakati wakienda kufanya mitihani ya urafiki katika shule nyingine.

Wanafunzi 32, walimu wawili na dereva walifariki dunia katika ajali hiyo.

Wanafunzi watatu, Doreen Mshana, Saidia Ismail na Wilson Elipokea walinusurika na kupelekwa Marekani kwa matibabu zaidi.

“Lakini pia nimezungumza na wenyeji wao waliofanikisha Safari yao ya Marekani!! Hakika Mungu ni mwema wameendelea kuimarika na wanaendelea vizuri! shukrani kwa madaktari na kila aliyetenga muda wake kuwaombea. Wazazi wao wanawasalimu na wanawashukuru kwa ushirikiano na maombi yenu.” Ameandika Masanja.

Mwananchi

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364